Uncategorized

KMC YAGOMEA KUSHUKA DARAJA, YATAJA MBINU WATAKAZOTUMIA KUBAKI

admin June 11, 2020 8:47 am

UONGOZI wa KMC umesema kuwa utapambana kwa nguvu zote kuhakikisha timu inabaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2019/20.


KMC ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 29 kibindoni ina pointi zake 33.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwary Binde amesema kuwa wapo tayari kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki ili kujikusanyia pointi nyingi zaidi.

“Kweli hatukuanza vizuri hilo lipo wazi ila kwa sasa tupo sawa kutokana na kikosi kuwa na muunganiko mzuri hivyo tutapambana kuona timu inabaki ndani ya ligi,” amesema.

Jana KMC ilimenyana na Azam FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na kutoshana kwa kufungana bao 1-1.
BALAA LA DAVID MOLINGA NDANI YA LIGI LIPO NAMNA HII YANGA: TUPO TAYARI KUIVAA MWADUI FC, WAMSHUKURU MUNGU KUWALINDA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply