Home Uncategorized MTIBWA SUGAR HAWATAKI UTANI,HESABU ZAO HIZI HAPA

MTIBWA SUGAR HAWATAKI UTANI,HESABU ZAO HIZI HAPA


UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umesema kuwa hesabu kubwa zilizo ndani ya kikosi hicho ni kuleta ushindani mkubwa kwenye mechi zilizobaki kwa kuwa wanaamini wana kikosi kizuri.

Mtibwa Sugar, iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila ina kibarua cha kumenyana na Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Juni 20.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kikubwa ambacho wanachokitazama ni ushindi kwenye mechi zao zote zilizobaki.

“Hatupo sehemu nzuri kwa sasa ni muhimu kupambana na lengo ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri ili kujiwekea nafasi nzuri zaidi,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA BETIKA, NAKALA YAKE NI BURE KABISA