Home Uncategorized BUSUNGU AFUNGUKIA USAJILI WAKE YANGA

BUSUNGU AFUNGUKIA USAJILI WAKE YANGA

MALIM Busungu, mchezaji wa zamani wa Yanga amesema kuwa amekuwa akiskia taarifa zake za kutakiwa na Yanga jambo ambalo limekuwa likimpa usumbufu kutoka kwa watu wake wa karibu.
Busungu aliwahi kucheza ndani ya Yanga  ambapo msimu wa 2015 alijiongezea umaarufu kwenye michuano ya Kagame kwa sasa hana timu baada ya kuachana na klabu yake ya Lipuli.
Akizungumza na Saleh Jembe, Busungu amesema kuwa amekuwa akipata msumbufu mkubwa kwa watu wengi wakitaka kujua kama anarejea Yanga ama la.
“Nimekuwa napokea simu nyingi ambazo zinauliza iwapo ninarejea tena Yanga, nashangaa hizi habari wanapata wapi? Mimi nipo ninaendelea na maisha yangi ila ikitokea watanihitaji siwezi kuficha,” amesema Busungu
SOMA NA HII  ISHU YA KAGERE NA SVEN IMEFIKIA HAPA