UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna kitakachowazuia kushinda mbele ya Mwadui FC baada ya kujipanga vema kwenye mchezo wa leo utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mchezo wao wa kwanza walifungwa na Mwadui jambo ambalo linawapa hasira ya kutafuta matokeo mazuri.
“Mchezo wetu wa kwanza tulichapwa hilo lipo wazi tunalijua,ila benchi la ufundi limejiandaa kupata matokeo mazuri kwa sasa tofauti na mwanzo.
“Ngumu kuamini kwamba kuna matokeo matatu, leo tunatambua aina moja ya matokeo ushindi hakuna kingine mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na ukweli ni kwamba mechi itakuwa saa 10:00 jioni na sio saa 11:00 jioni,” amesema.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 72 baada ya kucheza mechi 29, Mwadui FC ipo nafasi ya 12 na pointi zake 34 zote zimecheza mechi 29.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.