Uncategorized

MBAO WAJINYOOSHEA COASTAL UNION, BADO INA KIBARUA KIGUMU

admin June 24, 2020 5:47 am


MBAO FC jana imeinyoosha bao 1-0 Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Bao pekee la ushindi kwa Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro maarufu kama Baba Isaya lilipachikwa kimiani na Jordan John dakika ya sita lilidumu mpaka dakika ya 90 ambapo Coastal Union ilishindwa kufurukuta.

Wababe hao Coastal Union, chini ya mzawa, Juma Mgunda ambaye pia ana kibarua cha kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania anabaki na pointi 48 akiwa amecheza mechi 31 za Ligi Kuu Bara.

Ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara imebakiwa na mechi saba kukamilisha mzunguko wa pili.

Ngoma inabaki kwa Mbao FC kujinusuru nafasi iliyopo kwani licha ya ushindi huo imebaki nafasi ya 19 ikiwa na pointi  21 baada ya kucheza mechi 31.

Mchezo wa jana, Juni 23 ni wa kwanza kwa Minziro akiwa kwenye benchi la ufundi baada ya kupigwa chini mazima ndani ya Klabu ya Alliance FC.

Bado Mbao ina kazi ya kupambana kwenye mechi zake saba zilizobaki kumalizia mzunguko wa pili ili isishuke daraja jumla.

10 LEO KUSAKA POINTI TATU, YANGA USIKU SIMBA JIONI, RATIBA HII HAPA VIDEO: TAZAMA MABAO MAKALI MANNE, PRISONS V JKT TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply