AZAM FC, kesho ina kibarua cha kumenyana na Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Karume Mara.
Ikiwa chini ya Aristica Cioaba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.
Inakutana na Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza ambaye ametoka kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya KMC.
Kwenye mabao hayo manne, mshambuliaji wake Atupele Green alitupia mabao matatu na kusepa na mpira wake baada ya kufunga hat trick. Mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kupambana kufikia malengo yake.
Hesabu kubwa za Biashara United ni kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo huku Biashara United ikihitaji kumaliza ndani ya 10 bora.
Mchezo wao uliopita wa mzunguko wa kwanza, Biashara ilimalizwa kwa kutunguliwa mabao 2-1 jambo litakaloongeza ushindani hasa kwa kuwa Biashara Unted itakuwa kwenye utawala wake.
Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 huku Biashara United ikiwa nafasi ya tisa na pointi 43 zote zimecheza mechi 31.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.