Home Uncategorized ISHU YA LOGO NYEKUNDU YA SEVILLA, HAYA HAPA MAONI YA JEMBE

ISHU YA LOGO NYEKUNDU YA SEVILLA, HAYA HAPA MAONI YA JEMBE

[the_ad id="25893"]


ANAANDIKA Saleh Jembe kuhusu maoni masuala ya nembe ndani ya Klabu ya Yanga namna hii:-Nimezungumza mara nyingi sana kuhusiana na hili suala lakini WASIO NA HOJA akaishia kwenye Matusi, sasa leo TUJIFUNZE TENA.

ANGALIA LOGO ya Sevilla FC ina rangi nyingi nyekundu na leo Yanga wanaingia nao mkataba logo yao ikiwa na rangi zake.

Hapa nyumbani kampuni zote zilizoingia mkataba na Yanga kwa maana ya kuwa zinatoa fedha, bado Yanga walishindwa kuonyesha heshima na baadaye kulazimika kubadili rangi za logo zao.


 Mfano mzuri, wadhamini wa ligi Vodacom ambao Yanga wanafaidika nao… Angalia GSM PIA.

Utasikia sisi hatuwezi kufanya kazi na watu wenye rangi nyekundu.

Nimefafanua mara nyingi sana kuwa si kila nyekundu ni Simba au kila njano ni Yanga.

Wadhamini au partners wanapaswa KUHESHIMIWA na vizuri tukaacha “USHAMBA WA RANGI”… Hili la  Sevilla na La Liga linaweza kuwa funzo kwa wale ambao kweli hawakuwa wakielewa au wale walikuwa HAWAELEWI KWA MAKUSUDI..

SOMA NA HII  SENZO AMKATALIA SVEN, MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here