Home Uncategorized SIMBA:ITAKUWA KAZI NGUMU MBELE YA MWADUI FC ILA TUPO TAYARI

SIMBA:ITAKUWA KAZI NGUMU MBELE YA MWADUI FC ILA TUPO TAYARI


UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja Mkuu wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wapo tayari kwa kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui.

“Mchezo wetu uliopita mbele yao tulipoteza hivyo nasi pia tumejipanga kuona namna gani tutapata pointi tatu mbele ya Mwadui FC.

“Utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya kupambana na maandalizi yapo sawa kwani wachezaji wapo tayari,” amesema.

Bao pekee la ushindi kwa Mwadui FC lilifungwa na Gerald Mdamu ambaye ana mabao matano na pasi tatu za mabao.

SOMA NA HII  Yanga nayo yaikimbia As Vita, yajitoa Kagame

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here