Uncategorized

SASA UNITED INAWANIA UBINGWA

admin January 14, 2021 7:47 am

 BEKI wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, amesema anashangaa kuona mashabiki wa timu hiyo hawaamini, lakini ukweli ni kwamba sasa wanawania ubingwa.United walikaa kileleni kwa mara ya kwanza juzi baada ya kufanikiwa kuwachapa Burnley bao 1-0 na kufikisha pointi 36, tatu mbele ya Liverpool.

 

Neville amesema ameona kuwa kundi kubwa la mashabiki wa United hawaamini kama wanaweza kutwaa ubingwa lakini ukweli ni kwamba timu hiyo inaweza kufanya hivyo kwa kuwa sasa ipo kileleni.

 

β€œHuu ni ushindi mkubwa kabla timu hiyo haijavaana na Liverpool Jumapili ijayo kwenye mchezo mwingine mkubwa wa ligi hii.β€œNaona kuwa ni kitu kikubwa kwa kuwa ndani ya wiki sita nyuma usigeweza kufikiri kuwa United inaweza kufika hapa ilipo kwa sasa.

 

Lakini kwa jinsi walivyo na morali unaweza kuona jinsi ambavyo walikuwa wakishangilia wenyewe.β€œNafikiri mashabiki wa United sasa wanatakiwa kujua kuwa wanawania ubingwa na lazima wafikiri kuhusu hilo, sijui kwa nini hawaamini lakini naona morali ya timu ipo juu sana,” alisema Neville

 
WAWILI KUPIGWA PANGA NDANI YA AZAM FC MAZIMA TUISAPOTI TAIFA STARS IFANYE VIZURI CHAN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply