KIKOSI cha Simba ambacho utakiona leo Jumatano kikipambana na Azam FC kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kilipangwa jana Jumanne asubuhi baada ya kocha wao Sven Vandenbroeck kupanga iwe hivyo.
Kocha huyo amesema kwamba kwa siku nzima ya Jumatatu hakuwa na mawazo na mechi hiyo kwa sababu ya kujipa muda wa kupumzika baada ya kurudi Dar wakitokea Mbeya ambapo walipambana kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara, akaongeza kuwa Kikosi cha kuiangamiza Azam kipo tayari na wanasubiri kuchukua ushindi.
Simba inamenyana na Azam FC mchezo wa hatua ya robo fainali ambapo mshindi atamenyana na Yanga ambao tayari wameshamaliza kazi yao jana, kwa kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1.
Sven amesema:”Kikosi kitakachocheza na Azam FC kitakuwa kizuri na ninajua ninakutana na timu bora hivyo lazima nami nipange kikosi makini cha kazi,”.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.