KENNEDY Juma ni miongoni mwa mabeki wazawa ambao wana juhudi binafsi ndani ya uwanja katika kupambania timu wakati wa kutimiza majukumu yake.
Licha ya kwamba amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba ila amekuwa akionyesha utofauti kila anapopewa nafasi kufanya kazi yake.
Akiwa chini ya beki kisiki wa Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast na Erasto Nyoni mzawa, amekuwa mtiifu kutii maagizo anayopewa na kuwa hatua kwa hatua na yule ambaye atakabidhiwa ale naye sahani moja.
Kwenye mchezo wa jana, alikuwa chini ya Wawa, Julai Mosi mbele ya Azam FC,Uwanja wa Taifa alimbana mtupiaji namba moja wa Azam FC, Obrey Chirwa ambaye hakupata nafasi ya kufurukuta licha ya ubora wake kuwa juu.
Kibindoni Chirwa ana mabao 8 na pasi tatu za mabao ila hakuweza kuifunga Simba na kuwafanya watolewe hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.
Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Juni 20 dhidi ys Mwadui FC wakati Simba ikishinda mabao 3-0 alikuwa chini ya Nyoni.
Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgiji amesema kuwa wachezaji wake wengi wanazidi kuimarika taratibu jambo linalomfanya awe na chaguo la kubadili kikosi namna anavyotaka.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.