JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu England amesema kuwa haelewi kwa nini wachezaji walishindwa kuwa makini katika kufikiria jambo lililowafanya waruhusu kufungwa mabao 4-0 na Manchester City.
Mchezo huo wa Ligi Kuu England, ulichezwa Uwanja wa Etihad na walipewa heshima na City kabla ya mchezo kwa kuwa wameutwaa ubingwa baada ya kupita miaka 30.
Klopp amesema inaumiza kuona wachezaji wake wa Liverpool kupoteza umakini tangu kipindi cha kwanza ambapo waliruhusu mabao 3 ndani ya dakika 20.
Kevin De Bruyne dk 25 kwa penalti, Raheem Sterling dakika ya 35 na Phil Foden dakika ya 45 walizama kambani kipindi cha kwanza na kipindi cha pili Alex Oxlade Chamberlain alijifunga katika harakati za kuokoa hatari dakika ya 66.
“Tulipoteza umakini naona ni mbaya sana kwetu,wapinzani wetu walikuwa na spidi kuliko sisi. Wao wametumia nafasi zao sisi hatufanya hivyo,” amesema.
City ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 66 huku mabingwa Liverpool wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 86 wote wamecheza mechi 32.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.