Home Uncategorized SIMBA YATAJA SABABU YA KUSHINDA LEO MBELE YA NDANDA FC

SIMBA YATAJA SABABU YA KUSHINDA LEO MBELE YA NDANDA FC


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wana sababu zaidi ya tano zitakazowafanya washinde mechi zao zilizobaki ikiwa ni pamoja na ya leo dhidi ya Ndanda.
Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wana kazi ya kucheza mechi mbili nyanda za juu kusini ambapo ya kwanza itakuwa dhidi ya Ndanda FC, Uwanja wa Nangwanda Sijaona na ya pili itakuwa Julai 8, Uwanja wa Majaliwa dhidi ya Namungo FC.
Akizungumza na Spoti Xtra Sven alisema kuwa sababu kubwa ambazo zinamfanya aamini kwamba atapata ushindi kwenye mechi zake ni pamoja na upana wa kikosi alichonacho jambo linalompa fursa kuamua aanze na nani.
“Nina wachezaji wengi ambao wana ubora mkubwa, hao wananipa sababu ya kuamini ninaweza kushinda, uwezo wa kila mchezaji kuamua kutafuta matokeo ndani ya uwanja pamoja na ushirikiano ambao upo ndani ya timu.
“Pia baada ya kuwa mabingwa tumetimiza lengo la kwanza hivyo tutacheza bila presha kubwa uwanjani kwa kuwa hatuna cha kupoteza zaidi ya kutoa burudani na mwisho kabisa ni kwamba tunahitaji ushindi ndio maana tunaingia uwanjani,” alisema.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 79 baada ya kucheza mechi 32 za ligi inakutana leo na Ndanda iliyo nafasi ya 17 na pointi 35 zote zimecheza mechi 32.
SOMA NA HII  VIWANJA HIVI NI ADUI MKUBWA WA MAENDELEI YA SOKA TANZANIA