Uncategorized

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU KUMSAJILI BERNARD MORRISON

admin July 10, 2020 7:47 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna mpango na mchezaji matata wa Yanga, Bernard Morrison ambaye amekuwa akitajwa kuhitajiwa na Simba.

Ilikuwa inaelezwa kuwa Simba walikuwa wanahitaji huduma ya Morrison ambaye aliwatungua walipokutana Uwanja wa Taifa, Machi 8 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Simba wana wachezaji wengi wazuri na hawana mpango wa kumvuta ndani ya kikosi cha Simba.

“Hakuna, hakuna mpango wa Simba kuzungumza na Morrison, tunatambua kwamba tupo imara na hatuwezi kuzungumza na mchezaji huyo licha ya kwamba yupo vizuri.

“Ninawajua wachezaji wazuri ila hayupo kwenye mipango yetu kwa sasa hayo yanayozungumzwa ni maneno tu hamna kitu kingine,” amesema.

Chanzo:Wasafi 

JOSE MOURINHO AKASIRIKA KWELI KISA SARE YANGA KUTUA DAR LEO KUENDELEA KUIVUTIA KASI SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply