Home Uncategorized YANGA YATIA TIMU MORO, KESHO KUVAANA NA MTIBWA SUGAR JAMHURI

YANGA YATIA TIMU MORO, KESHO KUVAANA NA MTIBWA SUGAR JAMHURI


KIKOSI cha Yanga kimetia timu ndani ya mkoa Morogoro tayari kwa mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kesho, Julai 22, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Yanga ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar ambao nao wanazitazama kwa ukaribu pointi hizohizo ndani ya uwanja.

Kila mmoja ana malengo yake kwa sasa ambapo Yanga hesabu zake ni kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili kibindoni ina pointi 68.

Mtibwa Sugar hesabu zao ni kujiongezea uhakika wa kubaki ndani ya ligi kwani wapo nafasi ya 14 wakiwa na pointi 41.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wana imani watafikia malengo waliyojiwekea kwa kupata ushindi mbele ya Mtibwa Sugar.

“Mchezo wetu utakuwa mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya ushindani, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wapo kwenye nafasi ngumu hivyo pointi tatu ni muhimu kwao.

SOMA NA HII  YANGA YATAJA MITAMBO YA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO