UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa umempa ruhusa kocha wa timu hiyo, Aristica Cioaba raia wa Romania kusajili wachezaji kufikia hata 15 kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao ili kufanya vizuri msimu ujao.
Azam FC msimu huu imekuwa katika kiwango cha kupanda na kushuka huku ikiyeyusha mataji manne mkononi.
Ilianza na taji la Kagame, kisha Mapinduzi,Shirikisho na Ligi Kuu Bara ambalo lipo mikononi mwa Simba.
Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakazi amesema kuwa wamempa ruhusa Cioaba ya kufanya usajili wa wachezaji wengi hata kama watafika 15.
“Msimu unaofuata utakuwa ni msimu wa kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri tofauti na ilivyokuwa msimu huu ndio maana utaona kocha amepewa uhuru wa kusajili wachezaji wengi ambao anawahitaji hata ikiwa 15.”
Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 69 kete yake ya mwisho ni dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine Julai 26.