Uncategorized

EYMAEL NYOTA WAKE WAWILI WAMPASUA KICHWA

admin July 24, 2020 1:47 pm


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa atakuwa na wakati mgumu mbele ya Lipuli kwa kukosa huduma ya nyota wake Lamine Moro na Deus Kaseke.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lipuli utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji ushindi.

“Unajua mchezo wetu dhidi ya Lipuli utakuwa mgumu ukitazama nitakosa huduma ya wachezaji wangu wawili muhimu hivyo lazima tuwe katika wakati ambao sio mzuri.

“Lamine aliumia kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Kaseke yeye alionyeshwa kadi mbili za njano hivyo ataukosa jumla mchezo wetu dhidi ya Lipuli.

“Bado kuna mambo mengine yanaumiza ila hakuna namna tutapambana kupata matokeo chanya,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 69 huku Lipuli ikiwa na pointi 13 na pointi zake 44 kibindoni haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi ikiwa itapoteza mchezo huo huku Yanga ikipiga hesabu kuwania nafasi ya pili.

MTUPIAJI NAMBA MOJA MBAO FC AMLILIA MKAPA, ATAJA SABABU ZA KUMKUMBUKA JAMIE VARDY YEYE NI NYAVU TU EPL

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply