Home Uncategorized EYMAEL: SINA LAMINE MORO, KASEKE, MORRISON SIJUI ITAKUAJE

EYMAEL: SINA LAMINE MORO, KASEKE, MORRISON SIJUI ITAKUAJE


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kwa kuwa anahitaji ushindi na hana wachezaji wake muhimu ndani ya kikosi cha kwanza.

Leo Yanga inamaliza hesabu ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kumenyana na Lipuli ambayo inahaha kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi.

Yanga hesabu zao ni kupata ushindi ili kuweza kufikia malengo ya kumaliza ligi wakiwa nafasi ya pili huku mpinzani wake akiwa ni Azam FC.

Yanga na Azam FC zote zina pointi 69 baada ya kucheza mechi 37 huku wakitofautiana idadi ya mabao ya kufunga, Azam ina mabao 50 na Yanga imefunga mabao 44.

Lipuli wao wapo nafasi ya 13 na pointi 44 ikiwa watapoteza mchezo wa leo kubaki kwao itabidi wachungulie matokeo ya timu nyingine hivyo njia pekee ya wao kubaki ndani ya ligi ni kushinda mbele ya Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa yupo kwenye wakati mgumu kwa sasa kutokana na kutokuwa na nyota wake muhimu.

“Nipo kwenye wakati mgumu kwa kuwa sina wachezaji muhimu ikiwa ni pamoja na Lamine Moro yeye ni majeruhi, Kaseke ambaye ana kadi, Tshishimbi, Haruna, Balama hawa wote ni majeruhi.


“Yondani hata sijui yupo wapi, Morrison najua tabia yake inajulikana, sijui itakuaje bado tunapambana ili kupata matokeo lakini katika hili sina furaha kwa kweli,” amesema.

SOMA NA HII  MBADALA WA ZAHERA AANZA MIKWARA YANGA, ATOA SIKU SABA