Home Uncategorized KIUNGO WA YANGA MORRISON AOMBA APANGWE KIKOSI CHA KWANZA AIMALIZE SIMBA

KIUNGO WA YANGA MORRISON AOMBA APANGWE KIKOSI CHA KWANZA AIMALIZE SIMBA

[the_ad id="25893"]

 BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga, amesema kuwa anamuomba Kocha Mkuu, Luc Eymael ampange kwenye mchezo huo ili afanya kazi yake mbele ya Simba.

Yanga itamenyana na Simba, kesho Julai 12 Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
Morrison alikuwa na mvutano wa kimkataba na masuala ya nidhamu na baadhi ya viongozi wa klabu yake ila kwa sasa amesharejea kambini na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi.
Morrison amesema: “Nikipata nafasi ya kucheza nitaendelea kulinda heshima yangu na ya klabu, muhimu naomba Mungu niwe na afya njema kisha kocha anipe nafasi ya kucheza.

“Ninachohitaji ni sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono tangu nimefika hapa Tanzania, kama timu tunataka kuendelea pale tulipoishia.
  
 “Tunahitaji matokeo mazuri ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao, muhimu naomba kocha anipe nafasi kama nitakuwa fiti kiafya kisha mashabiki watuunge mkono katika mchezo huo muhimu.”
SOMA NA HII  AGUERO MTUPIAJI NAMBA MOJA NDANI YA CITY NA HESABU ZA KUSEPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here