Uncategorized

CHAMA ATIMIZA AHADI YAKE KWA VITENDO LEO AKABIDHI MILIONI MOJA KITUO CHA YATIMA

admin August 4, 2020 3:47 pm


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama leo Agosti 4 amekabidhi msaada wa Tsh.1milioni katika kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni, Dar es Salaam.

Hiyo ni sehemu ya utekeleza wa ahadi yake aliyoitoa jana Agosti 3 wakati anakabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Simba iliyotolewa na mdhamini mkuu, kampuni ya Sportpesa.

Chama ni kinara ndani ya Simba kwa kutengeneza pasi za mwisho ambapo ametoa jumla ya pasi 10 na kufunga mabao mawili.

Amehusika kwenye mabao 12 kati ya 78 ambayo yamefungwa na Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji.

Kikosi chake kimetwaa mataji matatu msimu wa 2019/20 ikiwa ni pamoja na ngao ya jamii, taji la Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho huku mchango wa Chama ukiwa ni mkubwa.

YANGA WATAJWA KUKAMILISHA DILI LA NYOTA MZAWA ALIYEKIPIGA HISPANIA MAMBO YA MSIMU WA 2020/21 LIGI KUU BARA YATAKUWA NAMNA HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply