Uncategorized

YANGA WATAJWA KUKAMILISHA DILI LA NYOTA MZAWA ALIYEKIPIGA HISPANIA

admin August 4, 2020 2:47 pm


FARID Mussa, mchezaji huru mzawa mwenye miaka 24 inatajwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga ili atue ndani ya kikosi hicho.

Mussa mzaliwa wa Morogoro, ndani ya uwanja nafasi yake ni kiungo mshambuliaji kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na CD Tenerife ya Hispania kufika tamati.

Mkataba wake uliisha Julai mwaka huu na hakupewa dili jipya la kusaini hivyo kwa sasa ni mchezaji huru.

Ana uzoefu na Ligi Kuu Bara kwa kuwa aliwahi kuitumikia Klabu ya Azam FC kabla ya kuibukia ndani ya CD Tenerife, Aprili 2016. 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa uongozi kwa sasa unaboresha kikosi ambacho kitaleta ushindani msimu ujao wa 2020/21 huku akigoma kuwataja wachezaji walio kwenye mazungumzo nao.

“Tupo kwenye mchakato wa kufanya usajili baada ya kuachana na wachezaji wetu wengine ndani ya timu, kuhusu kuwataja wachezaji watakaokuja kwa sasa siwezi kusema ila tutawatambulisha utaratibu ukikamilika,” amesema.

SVEN HATA HAELEWI HATMA YAKE NDANI YA SIMBA CHAMA ATIMIZA AHADI YAKE KWA VITENDO LEO AKABIDHI MILIONI MOJA KITUO CHA YATIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply