KIUNGO Cleophace Mkandala “iniesta” aliyekuwa anakipiga Tanzania Prisons amekamilisha idadi ya wachezaji watatu wapya ambao wamejiunga na Dodoma Jiji FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Pia nyota wengine ambao wamejiunga na Dodoma FC ni pamoja na Michael Chinedu aliyekuwa akikipiga ndani ya Alliance FC pamoja na Seif Karihe wa Lipuli wote wakiwa ni wachezaji huru.
Dodoma FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Mbwana Makatta, msimu wa 2019/20 ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na imekata tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.