Home Uncategorized WACHEZAJI 10 KIGENI RUKSA KUSAJILIWA BONGO

WACHEZAJI 10 KIGENI RUKSA KUSAJILIWA BONGO

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu vilabu vya soka nchini kuendelea kusajili wachezaji 10 wa kigeni, hatua iliyochukuliwa baada ya kuzingatia maoni ya wadau.

 

 Waziri mwenye dhamana ya michezo, Dkt. Harison Mwakyembe amesema idadi ya wachezaji wanaotakiwa kuanza kucheza itabaki chini ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

 

Pia amesema bado wizara kwa kushirikiana na BMT na wadau wa soka watakaa kujadili aina na viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na kuingia kucheza nchini.

 

“”Ni vyema pia aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka nje wawe na weledi, wawe na uwezo mkubwa. Angalau nchi zilizopo katika nafasi ya 50 kwa FIFA ndiyo tusajili huko hata wa daraja la kwanza, ingawa bado hii si sheria ni maoni tu,” amesema Mwakyembe.

 

Amesema kati watu 977 waliotoa maoni, watu 809 wametaka idadi ya wachezaji 10 wakigeni. Kando na hayo Wizara imeagiza watu wanaoajiriwa nchini wawe na ulazima wa kujifunza / kufunzwa lugha ya Kiswahili.

SOMA NA HII  HII ROBO FAINALI SIMBA, YANGA BADO KITENDAWILI