Home Uncategorized KAMATI INAYOSHUGHULIKIA SAKATA LA MORRISON YAAHIDI KUTENDA HAKI

KAMATI INAYOSHUGHULIKIA SAKATA LA MORRISON YAAHIDI KUTENDA HAKI


 MWENYEKITI  wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Elias Mwanjala amesema watatenda haki katika suala la Bernard Morrison dhidi ya Yanga. 
Mwanjala amesema kuwa kikubwa ambacho wanakizingatia ni haki kwa timu zote mbili pamoja na mchezaji mwenyewe.


Jana, Agosti 11 Mwanjala alisema kuwa sababu kubwa iliyochelewesha maamuzi ya kesi hiyo ni nyaraka moja kukosekana kwa upande wa Yanga na mchezaji mwenyewe Morrison.

Pia alisema kuwa kwa namna mwenendo wa kesi unavyokwenda mambo ni mwendo wa usawa kwa kila timu hivyo ni muhimu kwa wadau kuwa na subira.

Leo Agosti 12 kamati inatarajia kutoa majibu kuhusu maamuzi ya kesi ya Morrison ambaye yeye anasema kuwa ana mkataba wa miezi sita huku Yanga wakisema kuwa ana mkataba wa miaka miwili ambao aliongeza.

Pia alitangazwa kuwa mchezaji wa Simba, Agosti 8 hivyo timu zote mbili zinahusika kwenye kesi hiyo iliyoshika hisia za wadau wengi.
SOMA NA HII  VPL: MTIBWA SUGAR 1-0 YANGA