Home Uncategorized MTIBWA SUGAR YADAI KIBWANA ALIYESAJILIWA YANGA BADO NI MALI YAO

MTIBWA SUGAR YADAI KIBWANA ALIYESAJILIWA YANGA BADO NI MALI YAO

 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa beki mpya aliyetambulishwa na Yanga Agosti 9 bado ana mkataba ndani ya timu hiyo yenye maskani yake Morogoro.


Kibwana amesaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga ambayo ipo kwenye harakati za kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu wa 2020/21 akibeba mikoba ya Juma Abdul ambaye hajaongezewa mkataba.


Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa Kibwana bado ni mali ya Mtibwa hivyo wanafuatilia ili wajue imekuaje mchezaji ametambulishwa Yanga.


Kifaru amesema:-“Shomari kijana mdogo ni mali ya Mtibwa Sugar bado ana mkataba ndani ya timu na inaonekana alidanganywa huko alikokwenda kwa kuwa haelewi hatma yake lakini sisi tunafuatilia kwa ukaribu.


“Siwezi kusema ana mkataba wa miaka mingapi ila ninachojua mimi ni mchezaji wa Mtibwa Sugar, ninawasiliana na mtu wa sheria ndani ya timu ili ajue mambo yatakuaje,” amesema.


SOMA NA HII  MORRISON: JUMA ABDUL ASINGENIACHIA, NISINGEIFUNGA SIMBA