Uncategorized

SERIKALI YASHANGAZWA NA SAKATA LA MORRISON KUTUMIA MUDA MREFU

admin August 12, 2020 12:47 pm

 SERIKALI imesema kuwa inashangaa na suala la maamuzi ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison kucheleweshwa kutolewa hukumu.


Mwakyembe amesema kuwa suala hilo likifika mikononi mwaka atatumia dakika 10 kutoa maamuzi.

Sakata la Morrison limeanza kuskilizwa Agosti 10 na 11 ambapo hakukuwa na majibu kutoka kwa Kamati ya Hadhi za Wachezaji kuhusu mvutano wa kimkataba kati ya mchezaji huyo na timu yake ya Yanga.

Leo Agosti 12 pia linaendelea kuskilizwa kukiwa hakuna majibu yoyote licha ya jana kamati kuahidi kutoa majibu majira ya saa saba.

Waziri wa Michezo, Harrison Mwakyembe amesema kuwa anashangazwa na kuona namna mambo yanavyokuwa magumu kwenye maamuzi jambo ambalo linapoteza muda mwingi.

“Suala la mkataba lipo wazi inanishangaza kuona mpaka sasa hakuna maamuzi ambayo yametolewa mpaka sasa ndio maana inapelekea kuwe na taarifa kwamba ndani ya timu kuna viongozi ambao wana mapenzi na timu.

“Hii inanipa wasiwasi kuwa tuna matatizo hasa katika kusajili wachezaji, kitu gani ambacho kinawapa TFF kufanya maamuzi mpaka zinapita siku tatu, mbili hii haipendezi.


“Sisi Serikali haiwezekani kuingilia haya masuala ya kimkataba lakini ikishindikana basi tunapeleka Baraza la Michezo Tanzania, (BMT) ikishindikana kabisa wataniletea waziri ndani ya dakika 10 tu nitakuwa nimetoa maamuzi,” amesema.

GEITA FC NAO WASHUSHA MAJEMBE YA KAZI RASMI BEKI MBAO ASAINI MIAKA MIWILI AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply