ARSENAL imekamilisha usajili wa winga Willian raia wa Brazil kwa dili la miaka mitatu, leo Agosti 14.
Winga huyo ametua Arsenal bure kwa kuwa mkataba wake ndani ya Chelsea ulikuwa umekwisha na walikuwa kwenye mvutano kwa upande wa kuongeza dili jipya jambo lililomfanya winga huyo aamue kusepa.
Amedumu ndani ya Arsenal kwa muda wa misimu saba na amekabidhiwa jezi namba 12 ndani ya kikosi chake kipya kwa ajili ya mandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2020/21.
Mikel Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa anaamini kutakuwa na mabadiliko makubwa ndani ya kikosi chake baada ya kupata saini ya winga huyo mwenye uzoefu na Ligi Kuu England.
Frank Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa hana tatizo na winga huyo anaamini atafanya vizuri huko anakokwenda kwani uwezo wake upo wazi.
Arsenal imepata saini ya winga huyo mwenye miaka 32 ambaye amesema kuwa kilichomvutia kutua ndani ya Emirates ni pamoja na mafanikio ya timu hiyo kutwaa taji la FA.