HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa anatambua mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakuwa na ushindani mkubwa jambo linalomfanya aandae kikosi chake kwa umakini.
Namungo itakutana na Simba Agosti 30 na kufanya uwe mchezo wa nne kukutana na Simba uwanjani kwenye mechi za ushindani huku Namungo ikikwama kuibuka na ushindi zaidi ya kuambulia sare moja.
Kwenye ligi walikutana mara mbili ambapo Simba ilishinda mchezo mmoja Uwanja wa Mkapa kisha ikaambulia sare ya bila kufungana Uwanja wa Majaliwa na funga kazi ya tatu ilikuwa ni Sumbawanga, fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo Namungo ilifungwa na kuacha taji likiibukia Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe Thiery amesema:”Najua itakuwa ni mara yetu ya nne kukutana na Simba uwanjani, hakuna cha kuhofia kwa kuwa nami ninaandaa kikosi kama ambavyo wao wanaandaa kikosi kikubwa ni utayari na ushindani kwa kila mmoja.”
Agosti 30 sura mpya ambazo zitavaa uzi wa Namungo kwa mara ya kwanza na kukutana na Simba ni pamoja na Sixtus Sabilo ambaye alikuwa akikipiga Polisi Tanzania, Abdulhaman Humud alikuwa anakipiga Mtibwa Sugar.