BAADA ya Simba jana kushinda kwa ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine leo inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kwenye mchezo huo mabao mawili yalikataliwa ambapo moja lilikataliwa kwa upande wa Ihefu lilifungwa na Jordan John kipindi cha kwanza na bao la pili kukataliwa lilifungwa na Meddie Kagere kipindi cha pili kwa kile mwamuzi alichoeleza kuwa wafungaji walikuwa wameotea.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara anaandika namna hii:-Uamuazi sahihi usiozingatia matakwa ya sheria.
“Assistant Referee huyu lau asingekataa hili goli halali angetrend sana jana usiku na leo angeweza kuwa maarufu kuliko sare ya kwa Mkapa jana.
“Yes ,tayari alishawanyima Ihefu goli linalofanana na hilo before,(Kabla) na mjadala ungekuwa Simba imebebwa Mbeya but now story (lakini sasa stori ) ni mshika kibendera avurunda Sokoine Stadium.
“Maamuzi yake mawili ni ya hovyo ila yanabeba dhana kuu ya baadhi ya waamuzi wetu ya kupenda kubalance mambo uwanjani.
‘Yaan kwa kuwa baadae aliona alikosea kuwanyima goli halali Ihefu ni lazma arudishie na kwa Simba, yaan kukosea mara mbili au tatu na hata mara kumi kwao haina shida ili mradi.
“Ndio maana Bongo siku hizi huwezi kukuta mwamuzi katoa penati zaidi ya moja au mbili kwa timu moja katika mechi kwa kuogopa ataonekana anaibeba timu hata kama ni kweli wapinzani wametenda madhambi yanayostahili hizo penati.
“Na ikitokea katoa penati basi hiyo timu iliyopewa iwe makini, anaweza kufanya makosa nje kidogo ya Penati box, refa akafunika kuwa penati na pia mchezaji wao anaweza kufanya kosa linalostahili Yellow card( kadi ya njano) lakini mwamuzi akatoa strait red,(kadi nyekundu ya moja kwa moja)