Home Uncategorized SIMBA YATAJA MUDA ITAKAYOREJEA NAFASI YA KWANZA

SIMBA YATAJA MUDA ITAKAYOREJEA NAFASI YA KWANZA


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amebainisha kuwa licha ya kwamba wamepata sare kwenye mechi yao na Mtibwa Sugar hesabu zake ni ndani ya dakika 560 sawa na mechi sita wawe tayari wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara.


Kocha huyo ameongeza kwamba hayo ndiyo malengo yake na anajuwa wazi atayafikia licha ya kupata sare na Mtibwa Sugar, Septemba 12, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Simba kwa sasa ina pointi nne baada ya kushinda mechi moja na Ihefu na sare moja dhidi ya Mtibwa Sugar ya bao 1-1 ipo nafasi ya tano ikivutwa shati na Yanga iliyo nafasi ya sita baada ya kukamilika kwa mzunguko wa pili.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema kuwa plani zake kwa wakati huu ni ndani ya mechi zao hizo sita wawe tayari wanaongoza ligi na kujiweka eneo la kutetea ubingwa wao.

“Plani tulizonazo ni kuwa baada ya mechi kuanzia tano au sita tunataka kuona tunaongoza ligi.

“Tunajua haitakuwa rahisi lakini tutapambana kulifanikisha hilo, bila ya kujali aina ya matokeo ambayo tutayapata,” alimaliza Sven.

Leo Simba inaanza kujiwinda kwa ajili ya mchezo wake wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 20 na utakuwa ni mchezo wao wa kwanza ndani ya ardhi ya Dar kwenye ligi ndani ya msimu mpya wa 2020/21.
SOMA NA HII  ISHU YA CHAMA NA KANDA YANGA WAIKOMALIA, HUYU HAPA SAUTI YA MWISHO