Home Uncategorized AZAM FC WAKUBALI MUZIKI WA MBEYA CITY, WAAMUZI WATOLEWA CHINI YA ULINZI

AZAM FC WAKUBALI MUZIKI WA MBEYA CITY, WAAMUZI WATOLEWA CHINI YA ULINZI

 

LICHA ya Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City,  jana Septemba 20, uongozi wa matajiri hao wa Dar es Salaam umesema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwao mwanzo mwisho.


Bao pekee la ushindi lilifungwa na Ally Niyonzima dakika ya 25 kwa kichwa akiwa ndani ya 18 akimalizia kona iliyopigwa na Nivere Tigere.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa haikuwa rahisi wao kushinda kutokana na ushindani ambao waliupata kwa kuwa Mbeya City muda wote walikuwa wanasukuma timu mbele.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu kwetu pia kwa kuwa Mbeya City muda wote walikuwa wakipambana kusaka ushindi kama ambavyo tulikuwa nasi tukisaka ushindi.


“Kikubwa ambacho tumeweza kukifanya ni kuendelea pale ambapo tuliishia hivyo bado tuna kazi ya kufanya na mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kuwa vinara wa Ligi kwa mzunguko wa tatu baada ya kufikisha jumla ya pointi 9 kibindoni wakiwa wamecheza mechi tatu kufunga mabao matatu na kushinda zote.




Pia kwenye mchezo huo Polisi walilazimika kutumia nguvu kuwalinda waamuzi wa mchezo huo kwa kuwa mashabiki walivamia uwanja na kusababisha vurugu kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi wa mchezo huo.

SOMA NA HII  CHAMA ATWAA TUZO YA KIUNGO BORA VPL 2019/20, AWAPOTEZA KIKOTI NA MAPINDUZI