Home Uncategorized GWAMBINA FC: HATUJAPOTEZA MATUMAINI, TUTAFANYA VIZURI MBELE YA SIMBA

GWAMBINA FC: HATUJAPOTEZA MATUMAINI, TUTAFANYA VIZURI MBELE YA SIMBA

 


JACOB Masawe, nahodha wa Gwambina FC amesema kuwa kupoteza mchezo wao mbele ya Ruvu Shooting haijawatoa kwenye ramani wataendelea kupambana kwa ajili ya mechi zao zinazofuata ndani ya Ligi Kuu Bara.

 Gwambina ambayo imepanda ligi msimu huu ikitokea Ligi Daraja la Kwanza imecheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 huku ikipoteza mechi mbili na kulazimisha sare moja.


Ilianza kupoteza mbele ya Biashara United kwa kufungwa bao moja kisha ikalizimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Gwambina Complex, jana Septemba 20 iliyeyusha pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Mabatini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Massawe amesema kuwa matokeo waliyoyapata ni darasa kwao litakalowafanya wafanye vizuri mechi zao za mbele ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba.

“Mpira na matokeo yake ya ajabu kweli, hakuna namna tunakubali tumeshindwa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zinazofuata.

“Hakuna mchezaji ambaye anapenda kuona timu inashindwa lakini kwa kuwa hata wapinzani wetu nao wanajipanga kama sisi ndio maana matokeo yanapatikana uwanjani.


“Hatujapoteza matumaini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani timu ina maelewano makubwa na hakuna tatizo lolote ni mpira tu,” amesema. 

Gwambina FC itamenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa Septemba 26.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING, AJIBU, KAKOLANYA NDANI