Home Uncategorized FRAGA MAMBO MAGUMU SIMBA, KUIKOSA GWAMBINA FC

FRAGA MAMBO MAGUMU SIMBA, KUIKOSA GWAMBINA FC

 

GERSON Fraga kiungo mkabaji ndani ya Klabu ya Simba atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu kutokana na majeraha ya mguu wa kushoto aliyopata.


Maumivu hayo alipata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 20.


Kwa muda huo kiungo huyo atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 26.


Taarifa za daktari wa Simba Yassin Gembe zimeeleza kuwa hana majeraha makubwa ila atakaa nje kwa muda huo ili kuwa imara 

SOMA NA HII  KOCHA WA NAMUNGO AINGIA ANGA ZA MTIBWA SUGAR