Uncategorized

NAMUNGO WATUMA UJUMBE HUU KWA AZAM FC

admin August 23, 2020 9:47 am

 

ABDULHAMAN Humud maarufu kama Gaucho nyota mpya ndani ya Klabu ya Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo wa kirafiki dhidi ya Azam FC.

Humud amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar anacheza nafasi ya kiungo.

Nyota huyo amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya ushindani kwani maandalizi na mazoezi tumefanya kiasi cha kutosha tuna amini kwamba mchezo utakuwa mzuri na wenye ushindani mkubwa.

“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na kushuhudia ushindani ndani ya uwanja,” amesema.

Azam FC leo ni kilele cha Azam Festival ambapo kwa sasa mechi za utangulizi zimeanza viwanja vya Azam Complex.

SARPONG ACHEKELEA KUIBUKIA YANGA, ATOA AHADI HII IHEFU FC WAPO VIZURI, WAMALIZANA NA NYOTA HAWA SABA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply