Home Uncategorized AZAM FC: MUZIKI WA TANZANIA PRISONS SIO MWEPESI

AZAM FC: MUZIKI WA TANZANIA PRISONS SIO MWEPESI


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa una kazi ngumu ya kusepa na pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kesho, Septemba 26 Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba tayari imeshatia timu ndani ya Rukwa kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo kamili kumenyana na wapinzani wao Priosns na wanaamini kwamba haitakuwa kazi nyepesi.

“Tumefika salama huku Rukwa na maandalizi yanaendelea kwani utaratibu upo wazi kwamba siku moja kabla ya mechi tutafanya mazoezi kwenye uwanja ambao tutautumia rasmi kwenye mechi ya ushindani.


“Kwa sasa tunaamini kwamba hautakuwa mchezo mwepesi kwetu kwani wapinzani wetu wapo vizuri na wamekuwa kwenye maandalizi kwa muda mrefu hivyo ugumu upo hilo ni jambo ambalo tunalitambua.


“Licha ya kwamba kuna ugumu tuna malengo yetu ambayo tunahitaji ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu ili kuendeleza rekodi yetu,” amesema.


Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo mechi zake tatu za mwanzo imeshinda zote na kujikusanyia pointi tisa huku wapinzani wake ikiwa nafasi ya nane na pointi zake nne kibindoni.


Kipa namba moja wa Azam FC, David Kisu ameweza kukaa langoni kwenye mechi zote tatu ambazo ni dakika 270 bila kuruhusu nyavu zake kutikisika.

SOMA NA HII  HAWA WATAPIGA PENALTI, FAULO, KONA