BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara,(TPLB) iliweza kufungia baadhi ya viwanja kwa msimu wa 2020/21 na kupendekeza viwanja vingine vya kuchezea.
Mpaka sasa taarifa ambazo zimetolewa na TPLB kuna viwanja vitano ambavyo vimeshafungiwa kwa sababu mbalimbali huku vikipewa muda kufanyia marekebisho ikiwa ni pamoja na:-
Uwanja wa Karume
Septemba 13, Uwanja wa Karume uliokuwa unatumiwa na Biashara United ulifungiwa na siku 21 zilitolewa ili kufanyiwa marekebisho ikiwa ni sehemu ya kuchezea na ile ya kubadilishia nguo.
Bodi ya Ligi ilipendekeza Biashara United kuchagua Uwanja kati ya CCM Kirumba ama Nyamagana kwa ajili ya mechi za nyumbani.
Uwanja wa Mabatini
Septemba 25, Uwanja wa Mabatini ulifungiwa kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni kukosa sifa zilidhoainisha kwenye kanuni ya saba inayozungumzia uwanja na sheria namba moja ya mpira wa miguu inayozungumzia uwanja.
Mabatini uliopo Pwani ambao ulikuwa unatumiwa na Ruvu Shooting kwa mechi za nyumbani kwa sasa hautatumika na Bodi ya ligi iliamua kuwapa maamuzi Ruvu Shooting kuchagua Uwanja wa Azam Complex ama Uhuru kwa ajili ya mechi za nyumbani.
Ruvu ilichagua Uwanja wa Uhuru, Dar.
Uwanja wa Ushirika, Moshi
Septemba 26, Uwanja wa Ushirika Moshi ulifungiwa na Bodi ya Ligi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa umekosa sifa za kikanuni na kuitaka Polisi Tanzania kuutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wa Arusha kwa mechi za Ligi Kuu Bara.
Uwanja wa Jamhuri
Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro uliokuwa ukitumiwa na Mtibwa Sugar nao pia ulifungiwa kutakiwa kufanyiwa maboresho sehemu tatu abazo ziliainishwa ikiwa ni 1:-Sehemu ya kuchezea.(Pitch)
2.Vyumba vya kubadilishia nguo.
3.Sehemu ya kukaa wachezaji wa akiba na Maofisa wa mabenchi ya ufundi.
Gwambina Complex
Uwanja huu unatumiwa na Gwambina FC walipewa siku 21 kuufanyia marekebisho sehemu ya kuchezea pamoja na vyumba.