Home Uncategorized WACHEZAJI WAMPA KIBURI KOCHA MKUU WA SIMBA SVEN

WACHEZAJI WAMPA KIBURI KOCHA MKUU WA SIMBA SVEN


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri dhidi ya JKT Tanzania kwa kuwa kuna wachezaji wazuri.


Miongoni mwa wachezaji ambao amekuwa akipenda kuwatumia kikosi cha kwanza na wanampa matokeo chanya ni pamoja na Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Luis Miqussone, Meddie Kagere na Said Ndemla.

Simba inashuka uwanjani leo majira ya saa 10:00 Uwanja wa Jamhuri kumenyana na JKT Tanzania ikiwa ni mchezo wa raundi ya tano.

Sven amesema kuwa muda mrefu hawajacheza Uwanja wa Jamhuri Dodoma hivyo anaamini kwamba wachezaji wake watapambana kupata matokeo chanya.

“Utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani ukizingatia kwamba muda mrefu hatujacheza Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ila hilo sio tatizo kwa kuwa tunawachezaji wazuri kwenye kila nafasi.

“Kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu kwani kwa malengo ambayo tumejiwekea ili kufika pale ambapo tunahitaji tunatakiwa kufanya jambo moja tu nalo kushinda,” amesema.

Simba imecheza jumla ya mechi nne ikishinda mechi tatu na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, ina pointi 10 kibindoni inakutana na JKT Tanzania yenye hasira ya kupoteza mchezo wake uliopita mbele ya Coastal Union.


Coastal Union ilishinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wao wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


JKT Tanzania ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 4 kibindoni inakutana na Simba iliyo nafasi ya 3 na pointi 10.

SOMA NA HII  SIMBA:ITAKUWA NI MAAJABU KWELI KUFUNGWA NA YANGA TAIFA