Home Uncategorized BIASHARA UNITED MDOGOMDOGO WANAKUJA, MGORE ANA JAMBO LAKE

BIASHARA UNITED MDOGOMDOGO WANAKUJA, MGORE ANA JAMBO LAKE

 


MABAO manne pekee kipa namba moja wa Biashara United ameyaokota kwenye nyavu zake anaitwa Daniel Mgore.


Ni timu moja kati ya sita ambazo wamekutana nazo uwanjani iliyoweza kumpa tabu kipa huyu mzawa akiwa kwenye majukumu yake ambapo kwa sasa ana jumla ya clean sheet tano.


Ilikuwa ni mbele ya Simba, Uwanja wa Mkapa wakati ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 na kuyeyusha pointi tatu jumla.


Licha ya kwamba Biashara United imeshinda mechi nne na kulazimisha sare moja ya bila kufungana na Ruvu Shooting,  Septemba 27 bado mwendo wa safu ya ushambuliaji ni bao mojamoja.


Mwendo wake ulikuwa hivi:-Biashara United 1-0 Gwambina, Septemba 6, Uwanja wa Karume, Biashara United 1-0 Mwadui, Septemba 13, Uwanja wa Karume.


Simba 4-0 Biashara United,  Septemba 20, Uwanja wa Mkapa, Ruvu Shooting 0-0 Biashara United,  Septemba 27,  Biashara United 1-0 Mtibwa Sugar,  Oktoba 4,  Biashara United 1-0 Ihefu.


Ipo nafasi ya nne na pointi 13 kibindoni kinara ni Azam FC akiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi sita msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  KICHWA CHA SAMATTA NA KITUE KWENYE AKILI ZA WACHEZAJI WETU BONGO