Uncategorized

MAGUIRE ALIAMSHA WAKATI MANCHESTER UNITED IKIPIGA 4G

admin October 18, 2020 6:47 am

 


HARRY Maguire,  nahodha wa Manchester United dakika ya 23 aliweza kufuta makosa ya mchezaji mwenzake Luke Show aliyejifunga dakika ya 2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United.


Dakika 90 zilikamilika kwa United kusepa na pointi tatu baada ya kushinda kwa mabao 4-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa St.James Park.


Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Bruno Fernandes dakika ya 86 na Aaron Wan-Bissaka dakika ya 90 na lile la nne lilipachikwa na Marcus Rashford dakika ya 90+6.


Sasa United chini ya Ole Gunner Solskjaer ina kibarua cha kumenyana na PSG Oktoba 20 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaopigwa Uwanja wa Parc des Princes.

KOCHA YANGA ATAJA SABABU ZITAKAZOWAPA UBINGWA ARTETA ACHAPWA BAO 1-0 NA MANCHESTER CITY, AHOJI KUHUSU VAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply