Home Uncategorized C7 MUGALU WA SIMBA ATAKIWA KUFUNGA MABAO MENGI

C7 MUGALU WA SIMBA ATAKIWA KUFUNGA MABAO MENGI


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Sven Vandenbroeck amempa kazi maalum mshambuliaji wake raia wa DR Congo, Chris Mugalu, kuhakikisha anatumia kila nafasi ambayo anaipata kuifungia timu hiyo mabao mengi zaidi.

 

Mugalu anayekamatia nafasi ya nne kwenye chati ya wafungaji msimu huu na mabao yake matatu, amekuwa kwenye kiwango bora tangu ajiunge na Simba ambapo Jumamosi iliyopita alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege.


Akizungumza na Championi Jumatano, Sven alisema: “Tumekuwa tukipongezwa sana kutokana na namna ambavyo tunacheza soka la kuvutia na kufunga mabao mengi kwenye michezo yetu msimu huu, najua watu wengi wamekuwa wakivutiwa na kiwango cha straika wetu, Chris Mugalu kutokana na takwimu zake nzuri.


“Lakini kwa upande wangu bado sijaridhishwa na namna ambavyo Mugalu, na wachezaji wengine wanavyopoteza nafasi nyingi za wazi tunazozitengeneza uwanjani, hivyo ni lazima tuwape programu ya kuhakikisha wanatumia vizuri kila nafasi tunayotengeneza kufunga mabao,” alisema Sven.

 

Simba iliyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga, Rukwa kesho Alhamisi.

SOMA NA HII  VIDEO:NAMNA SHINDANO LA JISHINDIE GARI ILIVYOTINGA KITAA