News

WAKATI WAKIWA WANASHINDA KWA TABU..MORRISON AKOLEZA ‘SHIDA’ SIMBA..AFUNGUKA A-Z…

admin November 9, 2021 12:30 pm


KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amefunguka kuwa licha ya hali ngumu wanayokutana nayo mwanzoni mwa msimu huu, bado kikosi hicho kina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba, Jumatano iliyopita wakiwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo, na kufikisha pointi 11 katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga wenye pointi 15, michezo sawa.

Akizungumza na  Gazeti la Championi Ijumaa, Morrison alisema: “Ni kweli hatujawa na matokeo mazuri katika michezo yetu

iliyopita msimu huu kulinganisha na wapinzani wetu, lakini niwahakikishie kuwa bado tuna muda wa kubadilisha hili na kama wachezaji tunafanya kila jitihada kuhakikisha tunapambana kutetea kombe letu msimu huu licha ya upinzani mkubwa ambao tunatarajia kukutana nao kutoka kwa wapinzani wetu.”

JERAHA LA LYANGA LAZUA HOFU AZAM…AFANYIWA X-RAY…YABAINIKA KAVUNJIKA PUA NA …. DUH..SIO POA…KUMBE MATOLA NA HITIMANA HAWAJUI LOLOTE KUHUSU UJIO WA KOCHA MPYA SIMBA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply