news

DUH..SIO POA…KUMBE MATOLA NA HITIMANA HAWAJUI LOLOTE KUHUSU UJIO WA KOCHA MPYA SIMBA..

admin November 9, 2021 2:32 pm


UJIO wa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco raia wa Hispania ambaye amepewa dili la miaka miwili umewashtua makocha waliokuwa kwenye timu hiyo kwa kuwa walikuwa hawafahamu lolote kuhusu kuwasili kwake Bongo.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa makocha hao ilieleza kuwa Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi pamoja na Hitimana Thiery ambaye alikuwa ni Kaimu Kocha Mkuu wa Simba walikuwa hawajajui kuhusu Pablo.

“Makocha wameshtuka na ujio wa Pablo kwa kuwa hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba anaweza kuja kwa ajili ya kupokea mikoba ya Didier Gomes hivyo ni kama imekuwa ni jambo la kushtukiza.

“Kikubwa ambacho walikuwa wanajua ni kwamba atakuja kocha atakuja ila kujua kwamba ni siku gani na anatokea nchi gani hapo ilikuwa ni shida kwao,” ilieleza taarifa hiyo.

Alipotafutwa Matola ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema kuwa hawezi kuzungumza alipotafutwaMwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu hakuweza kupatikana.

WAKATI WAKIWA WANASHINDA KWA TABU..MORRISON AKOLEZA ‘SHIDA’ SIMBA..AFUNGUKA A-Z… MANARA TENAAH…AIBUA JIPYA YANGA..AMTILIA SHAKA DIARRA DJIGUI..ADAI HAWEZI ….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply