KLABU ya Ajax imeibuka na ushindi wa mabao 13-0 kwenye mchezo wa Ligi ya Uholanzi maarufu kama Eredivise leo Oktoba 24 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa De Koel dhidi ya Klabu ya VVV.
Ajax ikiwa ugenini ilianza kupachika bao la kwanza dakika ya 12 kupitia kwa Jurgen Elkelenkamp aliyepachika mabao mawili na lingine alipachika dakika ya 57.
Mwiba alikuwa ni Lassina Traore ambaye alipachika mabao matano dakika ya 17,32,54,65 na 87.
Kwenye idadi hiyo ya mabao 13 ni bao moja lilipatikana kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Klaas-Jan Huntelaar dakika ya 74 na alipachika bao jingine dakika ya 76.
Dusan Tadic alipachika bao moja dakika ya 44, Antony alipachika bao moja dakika ya 55, Daley Blind alipachika pia bao moja dakika ya 59 na Lisandro Martinez alipachika bao dakika ya 78.
Nyota wa VVV alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 52 ni Christian Kum na kuifanya timu yake kumaliza pungufu.
Kwenye msimamo Ajax ni vinara wakiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 6 huku VVV ikiwa nafasi ya 11 na pointi tano.