Home Uncategorized SIMBA KUSHUSHA WINGA MATATA

SIMBA KUSHUSHA WINGA MATATA

 


INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba upo katika mchakato wa kumshusha winga wa kimataifa wa Msumbiji, Pachoio Lau Há King ‘Lau King’ katika dirisha dogo la usajili msimu huu.

 

Lau King kwa sasa anakipiga katika Klabu ya UD Songo aliyokuwa akichezea kwa mkopo kiungo Luis Miquissone, raia wa Msumbiji kabla ya kujiunga na Simba akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

 

Lau King, ana uwezo wa kucheza wingi zote mbili huku akiwa na rekodi ya kucheza mechi za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika na mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa Simba wapo kwenye mchakato wa kusajili winga huyo huku wakiwa katika mipango ya kuachana na kiungo wa kimataifa wa Kenya, Francis Kahata ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni.


“Hilo suala lipo, japokuwa siku hizi mambo yamekuwa yakienda kwa siri sana kutokana na viongozi wanaoshughulika na usajili kuwa wachache halafu wamewekewa ulinzi.

 

“Wenyewe wanamhitaji kwa sababu mchezaji ana ukaribu na Miquissoine, ndiyo maana kumekuwa na imani kubwa ya kuweza kumpata na wamepanga wakati wa usajili wa dirisha dogo kufanya hivyo ingawa bado wana mvutano juu ya Kahata kwamba abaki au aondoke,” alisema mtoa taarifa.

 

Championi lilimtafuta katibu wa timu hiyo, Dk Arnold Kashembe ambaye alisema kuwa suala la usajili wa mchezaji yeyote kwa sasa bado siri kwa kuwa usajili bado haujafi kia, hivyo akili ipo katika mechi zao za ligi wanazotakiwa kucheza msimu huu.

 

“Taarifa zinaweza kuwepo na zikawa siri kwa sababu muda wa usajili bado haujafi ka na kama timu akili yetu tumeelekeza katika mechi ambazo zipo mbele yetu kwa sasa, hilo likifi kia wakati wake tutaweka wazi watu wajue,” alisema Dk Kashembe.

SOMA NA HII  MBEYA CITY WANAMAINGIZO MAPYA YA KUTOSHA MBALI NA TIMU ZA TPL, CHEKI ORODHA YAO HII HAPA