SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa bado hajajua sababu ya kupoteza mechi mbili mfululizo jambo ambalo linampa tabu katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Wakiwa ni mabingwa watetezi wameyeyusha jumla ya pointi nane ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 baada ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na ilipoteza mechi mbili ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 na mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0.
Timu zilizompa tabu Sven ni zile za majeshi ambazo muda wote wapo fiti asilimia 100 kwa kuwa kazi yao ni mazoezi, Tanzania Prisons na Ruvu Shooting.
Ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi saba za ligi kwa msimu wa 2020/21.
“Matokeo mabaya na hayafurahishi ila bado sijajua sababu ni ipi katika kupoteza mechi zetu, ile ya kwanza ilikuwa ni sehemu ya mchezo naona imejirudia tena mbele ya Ruvu Shooting.
“Bado hatujakata tamaa tuna amini kwamba tutarejea kwenye ubora wetu na tutafanya vizuri katika mechi zetu zijazo,” amesema.
Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Oktoba 31.