SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limelazimika kuahirisha fainali ya Ligi ya Mabingwa iliyokuwa ichezwe Novemba 6, 2020, kutokana na kucheleweshwa kwa pambano la marudio la nusu fainali baina ya Zamalek ya Misri na Raja Casablanca ya Morocco kufuatia wachezaji zaidi ya 10 wa Raja kupatikana na Covid-19.
Nusu fainali hiyo ilikuwa imepangwa kuchezwa jan, Oktoba 31 lakini kwa sasa itasubiri hadi wachezaji wa Raja wapone.
Fainali hiyo imesogezwa mbele ili kutoa fursa kwa mechi za kufuzu AFCON zitakozochezwa mwezi ujao.
Timu ya Al-Ahly imetangulia kwenye fainali ikisubiri mshindi kati ya Zamelek au Raja Casablanca ambapo katika matokeo ya mechi ya kwanza Zamalek anaongoza kwa bao 1-0.