TONOMBE Mukoko nyota wa Klabu ya Yanga ambaye ameibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo amesema kuwa bado ana mkataba na timu hiyo kwa sasa.
Jina la Mukoko limekuwa likitajwa kuingia kwenye rada za Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.
Mukoko amesema kuwa ana mkataba wa miaka miwili na Yanga hivyo taarifa zinazoeleza kuwa anaondoka ndani ya kikosi hicho ni za uongo.