FRANCISCO Roman Alarcon Suarez maarufu kama Isco, kiungo wa Klabu ya Real Madrid imeripotiwa kwamba anahitaji kuondoka ndani ya timu hiyo inayoshiriki La Liga.
Akiwa chini ya Kocha Mkuu Zinedine Zidane ameanza kwenye mechi tatu za La Liga huku akishindwa kuanza hata dakika moja kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo linalomkosesha raha.
Kwa mujibu wa Marca, Isco raia wa Hispania akili zake kwa sasa amezielekeza kwenye kutimkia ndani ya kikosi hicho ifikapo Januari ili akapate changamoto mpya kwa kuwa anaona kwamba yeye sio chaguo la Zidane.
Zidane amesema kuwa anatambua kwamba Isco anahitaji muda na hawezi kusimama kwenye njia yake ya kutaka kuondoka Januari kwa kuwa ni maamuzi yake yeye mwenyewe.
Ripoti zinaeleza kwamba timu ambazo zinahusishwa kupata saini yake ni Everton ambayo imekuwa ikihitaji kupata saini ya kiungo huyo mwenye miaka 28 ambapo anaweza kukutana na kocha wake wa zamani Carlo Anceotti.