IKIWA ametoka kusaini dili jipya la kuinoa timu ya Manchester City kwa miaka miwili, Pep Guardiola ameanza na kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tottenham Hotspur ambayo ipo nafasi ya kwanza na pointi 20.
Mabao ya Tottenham Hotspur inayonolewa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho yalipachikwa na Son Heung-Min dakika ya 5 na lile la pili lilipachikwa na Giovan Lo Celsso.
Mchezo huo wa Ligi Kuu England ulichezwa Uwanja wa Tottenham Hotspur na kuwafanya City wasiamini wanachokiona baada ya dakika 90 kukamilika kwa kuwa walifanya mashambulizi mengi ambayo hayakuwa na faida.
Manchester City iliyo na pointi 12 ikiwa nafasi ya 11 kwenye mchezo huo ilimiliki mpira asilimia 67 huku Spurs ikiwa na umiliki wa asilimia 33. Kwa upande wa mashuti matano yaliyolenga lango na Spurs ilipiga mashuti mawili.
Bao la Manchester City lililofungwa na Aymeric Laporte lilifutwa na mwamuzi Mike Dean kwa kile alichoeleza kuwa ilikuwa faulo kabla ya kufunga bao hilo.