VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa walipoteza mbele ya KMC kwa kuwa walizidiwa mbinu hasa kwenye ubora jambo lililowafanya wapoteza mchezo wao huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Azam FC Novemba 21 ilikuwa ina kazi ya kusaka pointi tatu muhimu ili kuongeza kasi ya kuongoza ligi ila ilikwama kwa kuyeyusha pointi zote tatu muhimu zilizobaki mikononi mwa KMC, wana Kino Boys.
Unakuwa ni mchezo wa pili kwa Azam FC iliyo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 11 na pointi zake kibindoni 25 sawa na Yanga ikiwa inaongoza kwa idadi ya mabao mengi ya kufunga kupoteza.
Mchezo wa kwanza , Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba kupoteza ilikuwa mbele yaMtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ilifungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Jaffary Kibaya.
Azam FC imefunga jumla ya mabao 18 na Yanga wao wamefunga jumla ya mabao 13 kibindoni.Huku Azam FC ikiwa imefungwa jumla ya mabao matano na Yanga imefungwa mabao manne.
Bao pekee la ushindi wa KMC lilipachikwa na Relliats Lusajo akitumia pasi ya Hassan Kibunda lilimshinda mlinda mlango namba moja wa Azam FC, David Kissu.
Kocha huyo amesema;”Kwenye mpira huwa inatokea wakati mwingine wachezaji wanashindwa kuwa bora katika mchezo ambao wanacheza hiyo ni sababu iliyotufanya tukapoteza,”.